Alhamisi , 22nd Feb , 2018

Jonas Malheiro Savimbi alizaliwa Agosti 3, 1934 huko Angola, baba yake akiwa ni mkuu wa kituo cha reli cha Benguela Rail way line na mhubiri. Wazazi wake wote wawili walikuwa ni wa jamii ya Ovimbundu, ambayo ilikuja kuwa msingi mkubwa wa Savimbi.

Jonas Savimbi

Savimbi alikuwa ni miongoni mwa Waangola wachache waliobahatika kupata elimu kubwa zaidi kwa wakati huo ambao nchi ilikuwa chini ya Wareno. Kwani alipata fursa ya kusoma kwenye shule za dini (Protestant schools), lakini pia alisoma na shule za wakatoliki. Akiwa na miaka 2 alipata fursa ya kwenda kusoma Ureno na kuhitimu elimu ya sekondari huko. 

Alipokuwa huko aliungana na vijana wengine kutoka Angola na nchi zingine ambazo zilikuwa koloni la Mreno, na kuanza kujiandaa na harakati za kupinga ukoloni , huku wakiwasiliana na chama cha kikomunisti cha Kireno. Alikuwa akifahamiana na Agostinho Neto ambaye kwa muda huo alikuwa akisoma medicine na baadaye kuja kuwa Rais wa kwanza wa Angola.

Savimbi aliondoka Ureno na kwenda Uswisi kwa msaada wa makomunisti wa Kireno na Ufaransa. Akiwa huko aliweza kupata fursa ya kusoma kwenye shirika la kidini la Marekani na kuchukua local science, na kisha kuendelea na masomo ya political science katika chuo kikuu cha Fribourg.

Akiwa huko mwaka 1960, alikutana na Holden Roberto ambaye tayari alikuwa maarufu kwenye harakati za kudai uhuru wa Angola kwa umoja wa Mataifa na muasisi wa chama cha UPNA. Alijaribu kumpa mafunzo Jonas Savimbi ambaye kwa wakati huo alikuwa akionekana bado hajafanya uamuzi wa kujitoa kabisa kwa harakati hizo.

Savimbi akapata uongozi baada ya kujiunga na MPLA , baadaye alitemwa na MPLA na kujiunga na FNLA mwaka 1964. Mwaka huo huo alianzisha UNITA akiwa na Antonio da Costa Fernandes . Savimbi alienda China kwa ajili ya kuomba msaada, na kuahidiwa silaha na mafunzo ya kijeshi.

Aliporudi Angola mwaka 1966, aliitambulisha UNITA huko na kuanza harakati zake kama mpiganaji mkuu wa kupinga utawala wa Kireno,  na pia alipamba na na FNLA na MPLA kupinga kusudio lao la kutaka kujiweka wenyewe kuiongoza Angola.

Kufuatia uhuru wa Angola Mwaka 1975, Savimbi alikuwa ameshajiwekea misingi mizuri kwa nchi kama China. Na kupewa misaada mbali mbali aliyokuwa akiihitaji kijeshi, na kuamua kuwa kama muasi kwa nchi yake, akitumia jamii yake ya wavimbundu kuwapa mafunzo na kupigana.

Savimbi alikuwa akipendwa na wanadiplomasia wa nchi mbali mbali ikiwemo Marekani ambao walikuwa na manufaa na migogoro ya Angola, huku akiweza kuongea kwa ufasaha lugha 7 tofauti duniani. Kutokana na mafunzo yake aliyoyapata, Savimbi aliwahi kutajwa kama muasi hatari zaidi kuwahi kutokea kwenye karne ya 19.

Baada ya kunusirka mashambulizi kibao ya kuuawa, na kutangazwa kufa zaidi ya mara 15,  Februari 22, 2002, Jonas Savimbi aliuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la Angola katika eneo la Mexico ambako ndiko alikozaliwa. Savimbi aliweza kuvumilia risasi zaidi ya 15 zilizompata sehemu mali mbali kichwani, kooni, miguuni , hakufa kirahisi mpaka pale alipoanza kujibu mashambulizi ndipo hali yake ikawa mbaya na kufariki.