Jumatano , 13th Mar , 2019

Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na wataalamu wa ujenzi wa uwanja wa soka unaotarajiwa kujengwa Jijini Dodoma.

Ramani ya Uwanja mpya wa soka utakaojengwa Jijini Dodoma

Mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na wataalam wa ujenzi wa uwanja kutoka Morocco na Tanzania pamoja na Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Abdelillah Benry, yameshuhudiwa Rais Magufuli akioneshwa ramani ya uwanja huo.

Baada ya mazungumzo na Rais Magufuli, balozi huyo wa Morocco amesema kuwa, " tumekuwa na mazungumzo kuhusiana na mipango ya maendeleo kati ya Morocco na Tanzania. Kwa sasa tuna miradi mikubwa miwili tunaisimamia, ambayo ni ujenzi wa msikiti pamoja na uzinduaji wa ujenzi wa Uwanja wa Soka", amesema balozi Benry.

Uwanja huo unajengwa kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco, Mohamed VI katika eneo la Nara Jijini Dodoma, barabara ya kuelekea Singida ambapo jumla ya hekari 143 zimetengwa. Unatarajia kugharimu sh bilioni 56 na ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji zaidi ya  85,000 hadi 100,005 watakaoketi kwenye siti.

Sambamba na ujenzi wa uwanja wa soka, pia kitajengwa kituo cha michezo ambacho kitakuwa kilomita 3 kutoka kwenye uwanja huo.

Pia inaelezwa kuwa ramani ya uwanja huo imetengenezwa kwa kulinganisha na mlima Kilimanjaro, ambao ndiyo mlima mrefu zaidi barani Afrika. 

Bonyeza hapa chini kuutazama uwanja huo.