Jumamosi , 15th Dec , 2018

Moja ya waliokuwa wanawania kupewa nafasi ya kugombea Urais kupitia kwenye Chama Cha Mapinduzi mwaka 2015, Dk Muzzammil Kalokola amedai atakuwa ni moja ya watu ambao wataonesha nia ya kugombea nafasi ya Urais kupitia Chama hicho mwaka 2020.

Chana Cha Mapinduzi

Kada huyo Mkongwe wa CCM, amedai moja ya sababu kubwa ambayo imemfanya aweke wazi hilo ni Mwenyekiti wao wa chama Rais John Magufuli amekuwa akikiuka baadhi ya taratibu za chama hicho ikiwemo kuteua wapinzani katika nyadhifa mbalimbali.

CCM tulijiwekea utaratibu wa kumuachia Rais kuwa mgombea pekee pale anapomaliza miaka mitano ili akamilishe mitano mingine ili kipindi chake cha miaka 10 kikamilike, lakini Rais Magufuli amekiuka misingi kwa hivyo hakuna sababu ya kumwachia, nitaomba ridhaa nipitishwe.” amesema Dk Kalokola.

Haiwezekani mtu ambaye wakati wa kampeni za kuwania Urais mwaka 2015 alikuwa akimtukana na kutumia njia zote kuhakikisha Magufuli anakosa urais, leo ametangaza kuingia CCM, kesho jina lake linapitishwa kugombea ubunge, kesho kutwa anakuwa waziri,” alisema Dk Kalokola.

Licha ya Kada huyo kuonesha nia ya kuwania nafasi ya Rais Magufuli, mwingine ambaye alikuwa ametajwa ni aliyekuwa Mbunge wa Mtama, Bernard Membe lakini taratibu za chama hicho zinakataza mtu kutangaza kuwania nafasi ambayo tayari inaongozwa na kiongozi wa chama hicho.