Jumamosi , 25th Jan , 2020

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano na Umma, Chama Cha Wananchi CUF, Abdul Kambaya amesema baada ya kutangaza kujiuzulu ndani ya Chama Cha CUF amesema atakuwa mfanyabiashara wakawaida.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano na Umma, Chama Cha Wananchi CUF, Abdul Kambaya

Kambaya ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital iliyotaka kufahamu baada ya uamuzi wake wa kujiuzulu wadhifa wake ndani ya CUF ni shughuli gani anaenda kuzifanya.

"Kabla sijajiunga CUF nilikuwa nilikuwa mfanyabiashara wa kawaida na niliingia pale nikiwa na gari zangu 4 natoa nikiwa na gari 2 kwa hiyo siasa sio shughuli bali ni wito." amesema Kambaya

"Nitaendelea kuwa mwanachama wa kawaida, huku biashara zangu zikiendelea" ameongeza Kambaya