Jumanne , 16th Feb , 2021

Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema kuwa huwa inao utaratibu wa kupuliza dawa ya kuuwa wadudu karibu maeneo yote ya hospitali na kwamba wakati wa zoezi hilo wagonjwa hutolewa nje na kuwekwa chini ya mahema.

Bango linaloonesha hospitali ya Taifa Muhimbili

Kauli hiyo imetolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa hospitali hiyo, baada ya picha kusambaa mitandaoni zikionesha vitanda vya hospitali hiyo vikiwa vimetolewa nje na kuwekwa kwenye mahema.

"Hospitali ina kawaida ya kupuliza dawa ya kuua wadudu mbalimbali wodini, maofisini na maeneo mengine ya nje mara mbili kwa mwaka, wakati zoezi likifanyika, wagonjwa  hutolewa nje na kuwekwa chini ya mahema huku huduma nyingine zikiendelea, hili ni zoezi la kawaida na endelevu", imeeleza taarifa hiyo