Jumanne , 26th Nov , 2019

Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Fredrick Sumaye, amesema kwa sasa hawezi kusema chochote kufuatia Kamati Kuu ya CHADEMA kupitisha jina lake peke yake kuwania Uenyekiti Kanda ya Pwani, bali atazungumza mara baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Kanda hiyo ut

Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Fredrick Sumaye.

Sumaye ametoa kauli hiyo leo Novemba 26, 2019, wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital, iliyotaka kufahamu maoni yake juu ya orodha ya wagombea walioteuliwa na chama hicho hivi karibuni.

"Kwa sasa siwezi kuwaambia chochote nitaenda kuwaambia hukohuko ndani, ila nikishapita naombeni mnitafute ndiyo nije, lakini kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu nikifanya hivyo nitakuwa nimefanya tambo za kampeni ambazo mimi sitaki kufanya" amesema Sumaye.

Uchaguzi wa kanda kwa chama hicho unatarajiwa kufanyika Alhamis ya wiki hii ambapo wagombea mbalimbali majina yao yamepitishwa na Kamati Kuu ya CHADEMA ili kuwania nafasi hizo.