Jumatatu , 15th Feb , 2021

Hospitali ya KCMC ya mkoani Kilimanjaro kupitia kwa msemaji wake Gabriel Chiseo, imeweka wazi kuwa hakuna mpango wa kugoma kwa madaktari kwenye ngazi zote na wanaendelea na majukumu yao kama kawaida.

Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro

Akiongea na Supa Breakfast ya East Africa Radio leo Februari 15, 2021, Gabriel Chiseo amesema, "Madaktari kwenye ngazi zote wote wako kwenye majukumu yao ya kawaida, hakuna mwenye wazo wala mwenye nia yakufanya mgomo" - Msemaji wa Hospitali ya KCMC Kilimanjaro, Gabriel Chiseo.

Aidha ameongeza kuwa, "Kwenye vifaa vya PPE sio kweli kuwa tumevikosa ama kuna uhaba hata kama kuna vifaa tunavikosa sisi huwa kuna namna tunavipata na hili halijawahi kutokea katika hospitali ya KCMC" - Msemaji wa Hospitali ya KCMC Kilimanjaro, Gabriel Chiseo.

Zaidi msikilize hapo chini