Jumatatu , 25th Nov , 2019

Idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya udongo na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini Kenya, imefikia 54 na kwamba idadi hiyo inahofiwa kuongezeka, kwani idadi kubwa ya watu bado hawajulikani walipo.

Picha si halisi

 

Jumatatu asubuhi, vikosi vinavyoshugulikia utafutaji miili ya watu waliofariki kwa kufukiwa na udongo na wengine kusombwa na maji, vinaendeleza shughuli hiyo, katika vilima vya Topach na Parua kaunti ya West Pokot, operesheni ikisitishwa mara kwa mara, kufuatia mvua kubwa inayozidi kunyesha eneo hilo.

Gavana wa West Pokot John lonyangapuo, ameitaka Serikali ya Kitaifa, kuingilia kati na kutafuta suluhu ya kudumu kwa mkasa huo ambao anasema haujawahi kutokea.

Katika Hospitali ya Rufaa Kapenguria, majeruhi wanaendelea kupata matibabu, watoto hawa, wasiwe na ufahamu kuwa mama yao hayupo tena, baada ya kufariki akijaribu kuwaokoa, kutokana na mkasa huo wa maporomoko ya ardhi, uliotokea usiku wa Jumamosi.