Jumatatu , 23rd Mar , 2020

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Ilala Milton Makongoro Mahanga, amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Ilala, Milton Makongoro Mahanga.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, asubuhi ya leo ya Machi 23, 2020, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, amethibitisha kutokea kwa msiba huo.

"Ni kweli aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Ilala na Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama amefariki asubuhi ya leo, alikuwa amelazwa tangu juzi Muhimbili, taarifa za kina zaidi tutazitoa baadaye" amesema Makene.

Milton Makongoro Mahanga, aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, katika Serikali ya awamu ya nne, chini ya Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.