Kigwangalla na Godwin Mollel wakagua Mobile Clinic

Jumapili , 31st Mei , 2020

Ndege ya abiria kutoka Shirika la ndege la Ethiopia inatarajiwa kutua Nchini kupitia Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro KIA Jumatatu ya Juni Mosi Mwaka huu ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ilipotangaza kufungua anga baada ya hapo awali kufungwa kutokana na Corona.

Waziri wa Maliasili na Dkt. Hamis Kigwangalla (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel (kulia).

Ndege hiyo inatarajiwa kuwasili ikiwa na abiria wanaoingia Nchini kwa shughuli mbalimbali zikiwemo Utalii na Biashara ambapo baada ya KIA ndege hiyo inatarajiwa kuelekea Visiwani Zanzibar.
 
Waziri wa Maliasili na Dkt. Hamis Kigwangalla pamoja naye Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakiwa na maafisa wa mamlaka za Utalii kutoka sekta za Umma na binafsi, wametembelea Kiwanja cha KIA na kueleza kuridhishwa na tahadhari zilizochukuliwa katika kuwakinga wageni na watumishi dhidi ya Corona.
 
Wakati huo huo viongozi hao wamekagua shughuli za utengenezaji wa Magari maalumu yanayotumika kama maabara zinazotembea kwaajili ya kuwahudumia Watalii yanayotengenezwa na kampuni ya HANSPAUL ya Jijini Arusha.
 

Zaidi Tazama hapo chini