Ijumaa , 16th Aug , 2019

Unapostaajabu kazi ya sanaa ilivyo, yakupasa kufikiria na ubunifu wa watengenezaji wa kazi zenyewe ikiwemo vinyago vyenye muundo wa aina mbalimbali.

Muuzaji wa kinyago chenye thamani ya milioni 50

Ukipita katika eneo la Mwenge Jijini Dar es Salaam, sehemu panapouzwa vifaa mbalimbali vya sanaa maarufu kama Vinyago, utakutana na kinyago kilichochongwa kwa zaidi ya miaka minne kuanzia mwaka 2008 na kukamilika June 2012, kinyago kilichomlazimu mchongaji kutumia akili kubwa zaidi ili kukimaliza.

Inaelezwa kuwa kinyago hicho kilichongwa na mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Joacqim Mpende, na mfanyabiashara wa kinyago hicho anaitwa Vitaly Katani, ambapo ameeleza kuwa bei ya kinyago chake kwa sasa ni milioni 50.

Inadaiwa wamekuwa wakipatikana wateja wa kukinunua, lakini changamoto iliyopo ni namna ya upatikanaji wa vibali vya kusafirisha kazi ya sanaa nje ya nchi.

Mtazame hapa akizungumza.