Alhamisi , 13th Jun , 2019

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango amebainisha kuwa kipato cha mwananchi mmoja mmoja kwa mwaka 2018 kimefikia Milioni 2.4 ikiwa sawa na ongezeko la asilimia 5.6 ukilinganisha kwa mwaka 2017.

Waziri Mpango amebainisha hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha hoja juu ya hali ya uchumi na mpango wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na 2019/2020.

Waziri Mpango amesema, "sekta zilizotoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa ni kilimo asilimia 28.2, ujenzi asilimia 13.0, biashara na matengenezo asilimia 9. 1. Mwaka 2018 pato la wastani la kila mtu lilifikia zaidi ya Milioni 2,458,496 sawa na ongezeko la asilimia 5.6".

"Kwa mujibu Ofisi ya Taifa ya Takwimu, pato halisi la taifa lilikuwa kwa asilimia 7.0 kwa 2018, ukuaji ulichangiwa na uwekezaji wa ujenzi wa miundombinu, kama viwanja vya ndege, na kuimarika kwa vyanzo vya umeme na kukua shughuli za burudani", amesema Dkt Mpango.

Leo Juni 13, 2019 Wizara ya Fedha inawasilisha Makadirio ya fedha na mpango wa maendeleo kwa mwaka 2019/2019.