Jumapili , 23rd Feb , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewaomba wafanyabiashara wa madini kutumia wakati huu kupigana kwaajili ya Rais Magufuli kwa kuyazungumza yale mazuri anayoyafanya pamoja na kuilinda amani ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Makonda ameyasenama leo Februari 23, 2020, katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini na kusema kuwa vita iliyombaya katika maisha ya watu ni ile ya uchumi kwani ziko silaha 11 zinazotumika kuangamiza nchi nyingi za Afrika, ikiwemo Demokrasia pamoja na ile silaha ya Kibiolojia

"Silaha ya Kibiolojia tunaweza tusiione kwa sasa, sasa mnaweza mkashangaa tukahangaika kutafuta dawa ya hawa wadudu Nzige wanaomaliza mazao, lakini kumbe kuna mtu amekaa Maabara kuwatengeneza wanaingia kwenye mashamba, watu wanakufa na njaa" amesema Makonda.

Aidha Makonda ametoa rai kwa yeyote atakayepata taarifa zilizo na mashaka, asisite kutoa taarifa kwenye vyombo husika.