Jumatatu , 15th Feb , 2021

Watoto wawili wamefariki dunia na watu wanne kunusurika kifo baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na kundi la fisi ambao wamekuwa wakiingia mara kwa mara vijijini, wakati wakitoka shambani  wilayani Nyang'hwale mkoani Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale Wilson Shimo

EATV ilifika Wilayani humo na kuzungumza na baadhi ya viongozi wa kijiji ambao wamesema matukio ya fisi kuvamia kaya za watu yamekuwa yakijitokeza mara nyingi hali inayopelekea wananchi kuishi kwa mashaka kwa kuhofia uhai wao.

"Hii hali ipo wiki mbili zilizopita hapo bupamba aliliwa mtoto wa mika kama nanae hivi na fisi usiku akamalizwa kabisa, yametokea matukio mawili moa nyaghamila na moja hapa izingwa, hukun lilishambuliwa watu wazima" amesema Mtemi Saleh Nzera Kiongozi wa Kimila.

"Jana nilipata habari kuna mtoto kangatwa na fisi akiwa anatoa mahindi ya kwenda kupika chakula cha jioni ilikuwa majira ya saa kumi na moja jioni akawa maejeruhiwa na yuko hospitalai anaendelea na matibabau kwahiyo hii hali inazidi kutodhoofisha katika mipango yoyote ya kimaendeleo" amesema Kafola Vicent Mwenyekiti wa Kitongoji Butalanda

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mariam Chaurembo amekiri uwepo wa kundi la fisi wanowashambulia watoto nakusema kuwa tayari wadau wanaohusika na wanyama pori washawasili wilayanai hapo kwa ajili ya kuwawinda na tiyari wameshakamata fisi sita akisema kuwa tiyari wameshawaruhusu wanakijiji kuiwawinda fisi hao ili waweze kuuwawa kutokana na kukithiri kwa matukio hayo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale Wilson Shimo amesema wameshatoa tahadhari kwa wananchi waweze kuwatunza watoto hususan katika kipindi cha jioni na asubuhi wasiwe wanatembea wenyewe.