Ijumaa , 15th Feb , 2019

Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imeanza kupiga kura ya maoni ya siri katika vijiji vyote vya tarafa tano za wilaya hiyo ili kuwabaini wahalifu wa matukio ya ubakaji na ulawiti ambayo yanaonekana kukithiri.

Kaimu katibu Tawala wa wilayani mufindi Joseph Mchina amesema kura ya siri ya maoni imeanza tangu Januari katika vijiji na mitaa na baadae litafanyika katika taasisi za elimu zikiwemo shule za sekondari, msingi na vyuo ili kuwabaini watu wanaohusika na matukio hayo.

"Siku ya Jumatatu tutakuwa na kikao na wakurugensi pamoja maafisa elimu pamoja na wadhibiti ili kuangalia namna ya kufanya shughuli hiyo bila kuathiri elimu" Amesema.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga  Charles makoga amesema kuwa sababu za matukio ya kikatili ya ubakaji na ulawiti katika mkoa wa iringa zinachagizwa na imani za kishirikina mambo ambayo yanatokana na ukosefu wa elimu.

"Watu wanawachukua vitoto vidogo hata vya miaka miwili, hata kama ni starehe kuna ladha gani pale zaidi ya kuwaharibu watoto. Nashanga hata haya mambo ya ubakaji yanawakuta hadi wasomi, Hivi kweli msomi unadanganywaje na mganga wa kienyeji? Biashara haifanikiwa kwa kubaka", amesisitiza.

Badhi ya wananchi waliozungumza na kituo hiki wamesema utaratibu wa serikali kupiga kura ya maoni ya siri uende sambamba na uandaaji wa takwimu sahihi kwa kuwa bado kunataarifa zilizipo hazina uhalisia na matukio.

Na Emmanuel mkulu