Jumatatu , 17th Feb , 2020

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limemtaka Mbunge Godbless Lema, kutoingilia kazi zake, kwani lazima litayatekeleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa huo, aliyetaka kukamatwa kwa waliohusika kusambaza video, zinazoonesha ubovu wa miundombinu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, bila kujali nafasi zao.

RPC Arusha, Jonathan Shana na kulia ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

Hayo yamebainishwa leo Februari 17, 2020, na Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Jonathan Shana na kusema kuwa Lema aache masuala ya kisiasa na kwamba badala ya yeye kushangaa kuona watu wakikamatwa kwa makosa ya kiuchochezi, bali Jeshi hilo litamshangaa yeye kwa kukosa uzalendo.

"Hili ni suala linalohusu uchumi wetu kwahiyo wanasiasa, wasilete masihara kwenye uchumi wa nchi, Mheshimiwa Lema na hii nasema kwenye dhati ya moyo wangu, kumtahadharisha akae mbali na suala hili wakati ambao jeshi lenye weledi likiwa kazini" amesema Kamanda Shana.

Jana Februari 16, 2020, Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Gambo, alitoa agizo hilo na kudai kuwa waliosambaza video hiyo wanayo nia ya kuhujumu uchumi wa Taifa.