Ijumaa , 21st Feb , 2020

Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema, amesema kuwa anao uhakika wa kuendelea kuwa Mbunge wa Arusha Mjini na kwamba hakuna mtu yeyote atakayeweza kuiba kura zake.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema

Lema ameyabainisha hayo wakati akizungumza na EATV &EA Radio Digital, ambapo pia ameonesha kushangazwa na Wabunge wanaohama upinzani na kuhamia chama tawala kwa kisingizio cha kwamba wanaenda kuunga juhudi.

"Hakuna mtu yeyeote atakayeweza kuiba kura, na mara hii tutashinda madiwani wote 25, kwanza CCM haipo hapa ndio maana imebaki biashara ya kurubuni, unabaki kujiuliza Mbunge aliyepo madarakani anamzuia nini Rais kutekeleza wajibu wake, kwani mimi siwezi kukuunga mkono lazima nije kwako, kwani nikifurahia ndoa yako lazima nije kulala kwako?" amesema Lema.

Lema ameyabainisha hayo wakati akijibu swali lilimhoji kwamba, haoni mvutano alionao kati yake pamoja na viongozi wa Serikali mkoani humo, akiwemo Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Jonathan Shana, unaweza ukamuathiri katika kipindi chake cha kampeni.