Alhamisi , 14th Mar , 2019

Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Maalim Seif kimesema kipo tayari kwa maamuzi yoyote yatakayotolewa na Mahakama ya kwamba nani atakuwa na uhalali wa kukiongoza chama hicho.

Kushoto ni Lipumba, Maalim Seif kulia.

Hayo yamesemwa na  Naibu Mkurugenzi wa Habari, wa chama hicho Maharagande Mbarala kwamba mpaka sasa chama chao bado hakijaitisha Mkutano Mkuu kwa kuwa wanasubiri maamuzi ya mahakama.

Akijibu ni kwanini mpaka sasa Mkutano huo haujaitishwa ilihali Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Lipumba amefanya Mkutano jana na kufanya Uchaguzi, Mbarala amesema uchaguzi Mkuu ulipaswa kufanyika mwezi Juni, hivyo muda wa uchaguzi, kama utafika kabla ya mahakama haijatoa maamuzi Katiba imewapa nafasi ya kuongeza miezi sita mbele.

Ameongeza kwamba Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif alishawahi kusema kwamba wataangalia cha kufanya baada ya mahakama kumtaja nani ni halali.

"Kama mahakama ikisema Lipumba ni halali kuwa Mwenyekiti tutakuja kujadiliana kuangalia namna gani ya kufanya, kama kumuachia chama alichopewa na mahakama au kukata rufaa. Lakini kama Lipumba hatakuwa na uhalali itabidi atupishe atuachie chama chetu", amesema.