Lowassa afunguka sakata la Lissu

Monday , 11th Sep , 2017

Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Edward Lowassa leo Septemba 11, 2017 amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu hospitali mjini Nairobi Kenya baada ya mbunge huyo kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017.

Edward Lowassa ambaye leo ameungana na baadhi ya watu wengine kwenda kumjulia hali kiongozi huyo amesema mbunge huyo sasa anaendelea vizuri na anaendelea na matibabu hata hivyo kiongozi huyo amesema kitendo alichofanyiwa Tundu Lissu ni kitendo cha kusikitisha kwa Tanzania.

"Mapema leo nilipomtembelea Mbunge, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na rafiki wa karibu Tundu Lissu, anaendelea vizuri kiafya, ila hizi ni nyakati za kusikitisha kwa Tanzania, kila mmoja kwa nafasi yake tuendelee kumuombea aweze kupona kabisaa" alisema Edward Lowassa 

Mbunge Tundu Lissu yupo nchini Kenye akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi tano na watu wasiojulikana  akiwa Makao Makuu ya Tanzania Dodoma.