Jumatatu , 10th Jun , 2019

Kamati Kuu ya Chama cha ACT-wazalendo iliyoketi Juni 9 na 10, imefanya uteuzi wa viongozi wa kitaifa ili kuboresha safu ya uongozi wa kitaifa wa chama hicho.

Maalim Seif alipokuwa akikabidhiwa kadi ya chama.

Miongoni mwa viongozi walioteuliwa ni pamoja na Maalim Seif Hamad ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mshauri Mkuu wa Chama, ikiwa ni moja ya ngazi kubwa katika chama hicho.

Viongozi wengine walioteuliwa katika mkutano huo ni, nafasi ya wajumbe wanne wa Kamati Kuu ya chama ambao ni, 1. Ndugu Theopista Kumwenda, 2. Ndugu Mwajabu Dhahabu, 3. Ndugu Fatma Fereji, 4. Ndugu Eddy Riyami. Wengine ni Wenyeviti na Makatibu wa Kamati za Kitaifa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Miradi ni ndugu Nassor A. Marzurui, Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ni Salim A. Bimani, Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi, Joram Bashange, Mwenyekiti wa Kamati ya Oganaizesheni, Mafunzo na Wanachama, Mhonga Ruhwanya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mikakati, Usimamizi na Ufuatiliaji, Ismail Jussa.

Ikumbukwe kuwa Maalim Seif pamoja na wafuasi wake walihamia ACT-wazalendo kutokea Chama cha Wananchi CUF kufuatia mgogoro wa muda mrefu ndani ya chama hicho.