Jumatano , 17th Feb , 2021

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad, amefariki dunia hii leo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa uhai wake

Taarifa za kifo hicho zimetolewa leo Februari 17, 2021, na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, na kusema kuwa kifo hicho kimetokea saa 5: 26 asubuhi, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

"Maalim amefariki wakati akiendelea na matibabu ambako alikuwa amelazwa tokea Februari 9 mwaka huu, kwa niaba ya wananchi natoa pole na salamu zangu za rambirambi kwa familia ndugu, jamaa, chama cha ACT Wazalendo na wanachi wote wa Zanzibar na kuwataka wawe wastahamilivu katika kipindi hiki cha majonzi makubwa, Taifa limepoteza kiongozi mzalendo na shupavu natangaza siku 7 za maombolezo", amesema Dkt. Mwinyi