Jumapili , 31st Mei , 2020

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro SSP Michael Stephen, amesema moto uliotokea usiku wa kuamkia leo Mei 31, 2020nje ya stendi ya Msamvu, haujaleta madhara kwenye usafiri.

Picha ya sehemu ya moto huo wakati ukiwaka

Akiongea na EATV&EARadio Digital asubuhi ya leo, SSP Michael Stephen amesema moto huo haujaleta madhara kwasababu umetokea kwenye vibanda vya nje ya stendi.

''Madhara makubwa kwenye usafiri hakuna kwasababu moto umetokea nje ya stendi ambapo umeunguza vibanda kadhaa pale lakini shughuli za usafirishaji ziliendelea kama kawaida'', amesema.

Aidha SSP Michael Stephen amewataka wananchi wenye vibanda eneo hilo kuwa na tahadhari ya matumizi ya moto.

Zaidi sikiliza mahojiano hapo chini