Jumanne , 14th Feb , 2023

Afrika Kusini imetangaza mafuriko yaliyotokea nchini humo kuwa  janga la kitaifa  baada ya mvua kubwa kusababisha majimbo yake saba kati ya tisa kufurika, kuharibu barabara na madaraja na kuwaacha wakulima wakipata hasara.

Maruriko hayo yamepelekea hasara kubwa kwa miundombinu na wakulima

 Taarifa kutoka ofisi ya Rais inasema ,Idara ya utabiri wa hali ya hewa inatabiri kuwa mvua kubwa itaendelea kunyesha.

''Serikali imetangaza hali ya kitaifa ya maafa ili kuwezesha kukabiliana na athari za mafuriko," ilisema taarifa hiyo, lakini haikutoa ishara yoyote ya idadi ya waathiriwa.

 Taarifa zaidi  Ilisema mvua kubwa ililetwa na hali ya hewa ijulikanayo kitaalamu kama  La Niña  , ambayo hutokea katika Bahari ya Pasifiki.

Taarifa hiyo iliongeza kuna uhitaji wa  utoaji wa makazi ya muda, chakula na mablanketi kwa familia zisizo na makazi na watu binafsi na ukarabati mkubwa wa miundombinu.

Wakati hayo yakijiri imetokea ajali nchini humo iliyoua Watu 20 waliuawa na wengine 61 kujeruhiwa kufuatia ajali kati ya gari lililokua likisafirisha fedha na basi katika jimbo la Limpopo nchini Afrika Kusini.

Basi hilo lilishuka kutoka darajani na kuingia mtoni , huku mvua kubwa zikileta changamoto ya vikosi vya dharura.