Jumatano , 19th Sep , 2018

Magari matano yameteketea kwa moto na mengine mawili  kuathirika na moto huo baada ya gari lenye namba za usajili T598 DCK kuwaka na kusambaa zaidi kiasi cha kupelekea hasara ya magari yote 7 yaliyokuwa yameegeshwa katika kituo cha mafuta Boko jijini Dar es salaam.

Pichani magari yaliyoteketea kwa moto.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Jumanne Murilo amesema kuwa moto huo umetokea majira ya saa saba usiku na bado wanafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

Gari saba zilikuwa zimeegeshwa eneo la kituo cha mafuta, bado tunafanya uchunguzi ili kujua nini chanzo cha moto huo”, Kamanda Murilo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa moto huo wameeleza kuwa moto umezuka majira ya saa 7 usiku na chanzo cha moto bado akijajulikana lakini wameeleza kwamba, gari moja ndio ilianza kiwaka moto yenyewe na kupelekea magari mengine kushika moto.

Wamesema kuwa gari lililoanza kuwaka moto pia lilijiendesha lenyewe likiwa linawaka moto na pelekea lori lililo upande wa pili kuanza kushika moto.

Gari yenye Namba za usajili T598 DCK ndio lilianza kuwaka moto yenyewe na kusambaa zaidi kiasi cha kupelekea magari yote 7 kuadhirika na moto huo", amesema mmoja kati ya shuhuda.

Tukio hilo linatokea ikiwa ni mwezi mmoja tangu magari matano ya mizigo kuteketea kwa moto katika kituo cha forodha Rusumo Wilaya ya Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda baada ya gari la mafuta ya petrol kuligonga gari jingine na kupoteza mfumo wa breki Agosti 19, 2018.

Tazama hapo chini muonekano ya magari yaliyoteketea.