Ijumaa , 18th Sep , 2020

Mgombea Urais wa tiketi ya Chama cha Mapinduzi,(CCM), Dkt.John Pombe Magufuli, amesema kuwa kazi ya kufufua zao la mchikichi ni kazi iliyotekelezwa chini yake na si kama wasemavyo wengine.

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiingia katika viwanja vya Lake Tanganyika nakulakiwa na Maelfu ya Wananchi waliyojitokeza kumsikiliza leo.

Amesema hayo leo Septemba 18 akiwa kwenye kampeni zake mkoa wa Kigoma ambapo amesema alimpa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kazi ya kufuatilia suala zima la ufufuaji wa zao la mchikichi.

"Nilimtuma Majaliwa natukaanza kufufua mashamaba ya JKT ili soko hili la mchikichi watu watajirike lakini nasikia kuna watu wanazungumza ndio wamefufua wao zao la mchikichi hapa jamani kwa hiyo nikituma mtu akishafanya vizuri mwingine anajitokeza pale" alisema Dkt Magufuli.

Aidha aliendelea kufafanua kuwa ufufuaji wa zao hilo la mchikichi ilikuwa kwenye moja ya mpango wa awamu ya uongozi wake kutokana na zao hilo kudharaulika.

"Tulivyoingia awamu ya 5 tuliamua kufufua zao la mchikichi hapa Kigoma kwasababu hili ndilo zao la biasahara hapa lakini likadharaulika na kusahaulika kwa siku nyingi “ alisema Dkt.Magufuli