Magufuli afanya uteuzi kwa Nassari

Jumatatu , 15th Apr , 2019

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Kikao cha Kamati Kuu kimemteua Ngugu, John Danielson Pallangyo kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Arumeru.

Rais Magufuli

Tume ya Uchaguzi ilitangaza uchaguzi wa marudio kuwa ni Mei 19 na Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa wazi baada ya aliekuwa Mbunge wake Joshua Nassari kuvuliwa ubunge na Spika kutokana na kutohudhuria vikao vitatu.

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika 2015, Pallangyo alikuwa mgombea wa Ubunge ambapo kwenye matokeo alishindwa na Nassari kutoka CHADEMA.

Chama cha Mapinduzi kimefanya Kikao cha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa NEC leo mchana jijini Dodoma wakiogozwa na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.