Magufuli amteua mbobezi wa uhandisi

Alhamisi , 11th Oct , 2018

Rais Dkt. John Magufuli, leo Oktoba 11, 2018 amefanya uteuzi kwa kumteua Dkt. Dalmas Lucas Nyaoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Uteuzi huo umeanza Oktoba 10, 2018.

Rais Magufuli

Dkt. Nyaoro ambaye ni mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika sekta ya uhandisi wa masuala ya Ardhi na teknolojia, (Geotechnical) akiwa na uwezo mkubwa wa kutatua matatizo makubwa ya fani hiyo kwa kutumia ufumbuzi wa vitendo na kinadharia.

Amefanya kazi katika nyanja zote za uhandisi wa 'Geotechnical', pia ni mtaalam mzuri wa uhandisi wa udongo, muundo wa udongo tata, mbinu za uboreshaji wa ardhi na maeneo mengine mbalimbali ikiwemo upimaji wa udongo katika maabara.

Dkt. Dalmas Lucas Nyaoro

Nyaoro ni mbobezi wa masomo ya Hydrogeological akimiliki PhD na MSc katika mitambo ya udongo kutoka Chuo cha Imperial (UK). 

Pia ni mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya wahandisi nchini, ambaye ni mwanachama wa Taasisi ya wahandisi Tanzania.
 

Taarifa ya Ikulu inaeleza zaidi hapo chini.