Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma
Ametoa wito huo leo Septemba 19, katika ufunguzi wa jengo la mahakama hiyo ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye.
"Napenda kutoa wito kwa majaji na watumishi kutunza miundombinu iliyojengwa, waswahili wanasema kitunze kidumu natoa wito kwa majajai kuhakikisha mahakama hii inatimiza malengo yake ya kujengwa" alisema Rais Magufuli
Aidha kwa upande wake, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, ameshukuru kwa nafasi aliyopewa ya kufungua jengo hilo huku akisema ni jambo la heshima sana kwake
"Ni heshima kabisa kwa mimi kuwa hapa na kunikubalia kufungua jengo hili zuri sana na hekima kubwa kwangu nawashukuru sana" amesema Rais Evariste Ndayishimiye.