Magufuli atuma salamu kwa Nape na Bashe

Tuesday , 14th Nov , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango afikishe salam zake kwa Mbunge Wabunge Nape Nnauye pamoja na Hussein Bashe  kuwa anawahitaji wawekezaji binafsi kwenye ujenzi wa reli

hivyo wampelekee.

Waziri Mpango ameyasema hayo akiwa bungeni na kusema kwamba Baada ya Wbunge hao kutoa maoni yao waliposimama kuchangia mapendekezo yao katika mpango wa maendeleo wa taifa na kukosoa serikali kutumia fedha zake katika miradi hiyo Rais Magyufuli alimpigia simu na kumpa maagizo hayo kwa wabunge hao wawili.

“Naomba ninong’one na Bunge lako tukufu. Mheshimiwa Rais Magufuli aliposikia huu mjadala, alinipigia simu na aliniambia hivi.. Waziri, mwambie ndugu yako mheshimiwa Nape na mheshimiwa Bashe kuwa nawataka sana hao wawekezaji kwenye ujenzi wa Standard Gauge Railway. Wawalete hata kesho niko tayari kuwapa reli ya kutoka Kaliua –Mpanda au Isaka-Mwanza au reli ya Mtwara-Mchuchuma hadi Liganga waijenge." Mpango

Mh. Mpango ameongeza kwamba Hayo ni maneno ya mheshimiwa Rais. Natumaini waheshimiwa husika wataifanyia kazi changamoto ya mheshimiwa Rais.”

Akifafanua kati ya hoja ambazo ziliibuliwa kuhusu kutowapa sekta binafsi nafasi Waziri Mpango amesema kwamba si kwamba Serikali imeiweka pembeni sekta binafsi bali  haijakaa vizuri na wakati mwingine inakuja na masharti yasiyotekelezeka.