Ijumaa , 18th Jan , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema hana uhakika endapo mrithi wake ataweza kutekeleza mambo anayoyafanya katika uongozi huu wa awamu ya tano.

Rais John Magufuli

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) iliyofanyika katika Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania(TCRA) jijini Dar es salaam. 

Amesema, "taifa hili ni tajiri, lina changamoto nyingi na changamoto hizo lazima tuzitatue sasa. Tusipozitatua kwenye awamu ya tano, hazitatatuliwa maishani, ninawaambia ukweli, changamoto zilizobaki sina hakika atakayekuja kama atazitatua".

"Sina hakika kwasababu katika kutatua unakutana na magumu mengi, ni mengi mno katika kuzitatua kuna magumu mno, na ndio maana inahitaji nguvu za Mwenyezi Mungu", ameongeza Rais Magufuli.

Akielezea faida za mfumo mpya wa takwimu za mawasiliano ya simu, Rais Magufuli amesema, utahakiki takwimu za mapato, takwimu za sauti, matumizi ya data na ujumbe mfupi, kujua simu za ulaghai pamoja na gharama za fedha za mtandaoni.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.