Mahakama yakasirishwa na kitendo cha Jamhuri

Thursday , 14th Sep , 2017

Mahakama imesema haijafurahishwa na kitendo cha Jamhuri kukataa kutekeleza amri yake iliyowataka mshtakiwa, Harbinder Sethi kupelekwa katika Hospitali ya Muhimbili kupatiwa matibabu ya tatizo lake la puto tumboni.

Wakili wa mshtakiwa huyo, Joseph Makandege amedai Mahakamani hapo kuwa mteja wake asipopatiwa matibabu ya puto lililowekwa tumboni kwa muda muafaka linaweza kupasuka na kupoteza uhai wake.

Aidha, Wakili huyo ametaka mshtakiwa namba moja ambaye ni Sethi apelekwe katika hospitali ambayo ina wataalam, waliobobea kwa madai Hospitali za Magereza hazina wataalam wabobezi juu ya tatizo la mteja wake.

Kutokana na hayo kesi imeahirishwa na kusikilizwa tena hadi Septemba 29, 2017.

Mfanyabiashara Harbinder Sethi anatuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha