Jumamosi , 15th Dec , 2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya Majiji hapa nchini, ikiwemo ya Dar es salaam, Tanga, na Arusha ili yaweze kuvutia watalii pindi wanapokuwa wanaingia nchini.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

"Lazima tutumie maeneo ya wazi kutangaza vivutio vyetu tulivyokuwa navyo, tukaona jitihada za usafi zikifanyika japo sasa hivi zimeachwa naangiza tuimarishe bustani zetu hapa za Dar." Amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Akizungumza Jijini Dar es salaam Waziri Mkuu Majaliwa amesema si sawa kuona jiji kama la Dar es salaam watali wanaingia nchini halafu Jiji la Dar es salaam linakuwa halifanani kuwa Jiji.

"Nguzo zote za taa ziboreshwe ziwake usiku ili zipendezeshe usiku kwa wageni wanaoingia usiku, unaingia jijini Dar es salaam jiji liko giza, haiwezekani wametushinda wafanyabiashara binafsi wanatushinda kutangaza juice na Ice Cream halafu sisi hatutangazi utalii." - alisema.

"Naagiza mikoa na Majiji mengine ambayo iko tayari kuboresha maeneo yao yatakayotumika kwa ajili ya utalii."