Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Kwa sasa Mji wa Wuhan umewekewa zuio hakuna mtu anayeruhusiwa kutoka wala kuingia, lengo likiwa ni kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.
Ametoa kauli hiyo leo Februari 16, 2020, kwenye Kumbukumbu ya Mazazi ya Mtume Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam iliyoandaliwa na Nida Textile Mills (T) ltd, na kufanyika katika Mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema kutokana na zuio hilo wakazi wote wa mji huo wakiwemo vijana wa Kitanzania, wanapata huduma mbalimbali kupitia njia ya mtandao.
"Hakuna usafiri hata wa umma unaofanya shughuli za kusafirisha watu katika mji wa Wuhan kila mmoja anaetakiwa abakie katika makazi yake na kwamba Serikali ya China na uongozi wa vyuo unawatunza wanafunzi wote wakiwemo na Watanzania" amesema Waziri Mkuu.