Ijumaa , 19th Mei , 2017

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kuuwa Majambazi watatu pamoja na kufanikisha kupatikana kwa silaha mbili wilayani Nyamagana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, amesema, majambazi hao wamefariki dunia wakiwa njiani kupelekwa hospitali kutokana na majeraha waliyopata baada ya kukabiliana na Polisi saa 2:30 usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Saint Mary Mtaa wa Ndofe Wilaya ya Nyamagana

Kamanda Msangi amesema, awali walimkamata mganga wa kienyeji aitwaye, Ayubu Nyamweru mkazi wa katoro mkoani Geita, akiwa na Kompyuta Mpakato tatu ambazo ziliibiwa katika tukio la kuvunja nyumba.