Majina yatajwa waliofariki kwa ajali ya Treni

Jumatatu , 23rd Mar , 2020

Wafanyakazi watano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRC), wamefariki dunia kutokana na ajali ya Treni ya uokoaji kugongana uso kwa uso na Kiberenge, katika eneo la Mwakinyumbi na Gendagenda mkoani Tanga.

Treni

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa TRC Jamila Mbarouk na kusema kuwa ajali hiyo imehusisha watumishi sita wa shirika hilo, ambapo wanne walifariki papo hapo na wawili walifikishwa katika hospitali ya Wilaya ya Magunga, Korogwe ambapo mmoja naye alifariki.

Taarifa hiyo imeyataja majina ya waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Ramadhan Gumbo, ambaye alikuwa ni Meneja usafirishaji Kanda ya Tanga, Mhandisi Fabiola Moshi ambaye alikuwa ni Meneja ukarabati wa mabehewa ya abiria kanda ya Dar es Salaam, mwingine ni Joseph Komba ambaye alikuwa ni Meneja Msaidizi usafirishaji kanda ya Dar es Salaam.

Wngine ni Philibert Kajuna ambaye alikuwa ni Mtaalam wa usalama wa Reli na George Urio ambaye alikuwa ni dereva wa Kiberenge, ambapo uchunguzi unafanyika ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.