Jumamosi , 20th Jul , 2019

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano Mazingira January Makamba, amesema, Serikali itaweka utaratibu wa kuziondoa chupa za plastiki, ambazo hazina soko na  haziwezi kurejereshwa upya, kwa kuwa zinaonekana kuzagaa na kuchafua mazingira.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano Mazingira January Makamba

Waziri Makamba ameyabainisha hayo Julai 20, alipotembelea kiwanda cha uzalishaji wa  vifungashio vya karatasi.

''Ukienda kwenye mifereji na fukwe, utakutana na chupa nyingi ambazo hazikusanywi kwa sababu hazina soko, na miezi ijayo tutaweka utaratibu wa kuwalazimisha waingizaji na wazalishaji wa chupa hizo  kuziondoa chupa hizi kwenye mazingira'' amesema Makamba.

Aidha Makamba amekisisitiza kiwanda hicho, endapo kutazalisha vifungshio hivyo kwa ajili ya soko la ndani, kitarahisisha upatikanaji wa bidhaa hiyo, ukizingatia Serikali imepiga marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki.