Ijumaa , 14th Dec , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Desemba, 14, 2018, amezindua kampeni ya utoaji wa kinga ya Matende, Minyoo, Mabusha na Kichocho kwa wa wakazi wa mkoa huo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda

Katika uzinduzi huo Mh. Makonda amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata kinga ili kujiepusha na magonjwa hayo.

''Ndugu zangu niwaombe tujitokeze kupata kinga hii, maana itatolewa kwenye vituo zaidi ya 923 ikiwemo Vituo vya afya, Mashuleni, Ofisi za watendaji Kata na mitaa, Vituo vya mabasi na Sokoni lengo ni kuwafikia wananchi wote'', amesema.

Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa kama mkoa wamekusudia kuwafikia zaidi ya wananchi 5,600,000 sawa na 100% ya wananchi wenye uhitaji wa kupatiwa kinga hiyo katika mkoa wa Dar es salaam.

Aidha Makonda ameipongeza Sekta ya afya kwa kazi kubwa wanayoifanya katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.