Jumanne , 16th Apr , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaasa wanafunzi kuachana na mitandao ya kijamii badala yake kuzingatia masomo ili waweza kufikia malengo waliyojiwekea .

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

RC Makonda ameyazungumza hayo alipokuwa akizungumza  na Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya  Mzimuni alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi yote iliyopo ndani ya Mkoa huo ambapo ametembelea shule hiyo kuona ujenzi wa madarasa 6, unaoendelea.

Amesema ili waweze kufanya vizuri katika masomo wanatakiwa kuweka juhudi, nidhamu pamoja na kuheshimu malengo yao waliojiwekea ambapo amewataka wanafunzi hao kufanya vizuri ili Rais Dkt. John Magufuli kuweza kujivunia  kuzalisha wanafunzi bora  katika nchi yake.

Mnauwezo mkubwa sana wakufanya vizuri achaneni na tabia za kukaa kwenye mitandao ya kijamii wekeni bidii kwenye masomo ili mje kulisaidia taifa, kuna mambo matatu ukiwa nayo lazima utafanya vizuri unatakiwa kuwa na juhudi, nidhamu pamoja na malengo, malengo yako lazima yawe tofauti na Dunia” amesema RC Makonda.

Amesisistiza kuwa wanafunzi wengi wamekiwa wakifuatilia mambo ya dunia jambo linalopelekea kufanya vibaya katika masomo.