Alhamisi , 11th Jun , 2020

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka wanaotangaza kuwa Dar es salaam sio sehemu salama waache mara moja kufanya hivyo huku akiwaomba Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA), kuruhusu wasanii wa Dar es salaam kufanya matamasha.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda

Makonda ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini, ambapo amesisitiza mambo mbalimbali ikiwemo kutoa onyo kwa watu wanaoichafua Dar es salaam.

''Nashindwa kuelewa nia ya watu wanaosema Hospitali zimefurika wagonjwa wa Corona wakati nchi yetu Mungu ameiokoa na tunaendelea na maisha na sasa nchi mbalimbali zimeanza kutuiga sisi, naomba sana watu wanaofanya hivyo waache'', amesema.

Aidha Makonda amesema hali sasa imeshakuwa shwari na pengine Baraza la Sanaa nchini liangalie uwezekano wa kuwaruhusu wasanii wa Dar es salaam waanze kufanya matamasha ili wajipatie kipato.

Zaidi Tazama Video hapo Chini