Jumatatu , 16th Apr , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa tahadhari kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuchukua tahadhari kwa mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo na kuwataka kukaa maeneo salama kwa ajili ya usalama wao na mali zao kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari, Makonda amesema kuwa utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa leo Aprili 16, 2018 mvua hizo zitakua kubwa zaidi hivyo wananchi hawana budi kuchukua tahadhari mapema zaidi.

"Katika mvua hizo zilizonyesha kwa muda wa siku mbili mfululizo zimeshaleta madhara kadhaa katika baadhi ya maeneo hivyo ili madhara zaidi yasiweze kujitokeza wakazi wa Mkoa huo wa Dar es Salaam hawanabudi kuchukua tahadhari mapema zaidi", amesema Makonda.

Kwa habari kamili sikiliza hapa chini.