Jumamosi , 23rd Mar , 2019

Waziri wa nchi  ofisi ya  Raisi Tawala za mikoa na serikali  za mitaa TAMISEMI Selemani Jafo ametoa wiki moja kwa wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Morogoro na nchini kwa ujumla, kuhakikisha wanatoa taarifa za fedha za mikopo ya asilimia kumi inatolewa kwa akina mama,vijana na walemavu

Selemani Jafo

Waziri Jafo ametoa agizo hilo wakati wa kongamano la vijana kujadili fursa za mkoa wa Morogoro ambapo amesema serikali imetoa maagizo kwa wakurugenzi wote nchini kuhahikisha wanatenga asilimia kumi ya mapato ya ndani kuwasaidi makundi maalumu ambayo ni akina mama ,vijana na walemavu jambo ambalo baadhi ya wakurugenzi wamekuwa hawafanyi.

Jafo amewataka wakurugenzi kuziwasilisha ripoti hizo kwa katibu tawala wa mkoa huo ili kutambua ni kiasi gani ambacho kimetolewa na kuwafikia walengwa.

Aidha Waziri Jafo ametoa muda wa miezi mitatu kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha fedha ilizotengwa kwaajili ya vikundi vya vijana, wanawake na walemavu zinawafikia walengwa ikiwa ni katika kutekeleza sheria ambayo Mheshimiwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameipitisha kwa lengo la kuwainua kiuchumi watanzania ambao asilimia kubwa ni wanyonge.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Omary Mgumba amewataka wakazi wa Morogoro  kutumia fursa za viwanda vinavyoanzishwa katika mkoa huo kujikita katika kilimo ili kuwakomboa kiuchumi.