Jumatano , 9th Nov , 2022

Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir, amewaagiza viongozi wa dini hiyo nchini kuwa siku ya Ijumaa ya Novemba 11, 2022, ni siku maalum kwa waislamu na Watanzania wote kumuomba Mungu mvua yenye heri na isiyokuwa na madhara.

Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir,

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 9, 2022, Sheikh Mkuu amesema kitaifa maombi hayo yatafanyika katika msikiti wa makao makuu ya BAKWATA yaliyopo Kinondoni na yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini

Aidha Mufti amesema watafanya dua ya kumuonba Mungu kuiepusha nchi na balaa la ajali mbaya zikiwemo za ardhini , majini na angani na kuendelea kuipa amani nchi ya Tanzania

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameunga mkono hatua hiyo na kusema kwamba kwa hali ilipofikia kwa sasa kuna kila sababu ya kumuomba Mungu ili awaepushe Watanzania na majanga ya ukame.