Mapya yaibuka Mganga aliyembaka mgonjwa wake

Jumatatu , 13th Jan , 2020

Siku chache baada ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, kumkamata mganga wa kienyeji anayefahamika kwa jina la Hemed Jumanne mkazi wa wilaya ya Sengerema kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa wake wakati akimtibu.

Mazingira ya Mganga wa kienyeji.

Chama cha waganga wa tiba asili na tiba mbadala mkoani Mwanza (CHAWATIATA), Kata ya Kishiri kimelaani vikali kitendo kilichofanywa na mganga huyo na kuahidi kutofumbia macho vitendo vya udhalilishaji wa taaluma hiyo.

Mganga huyo wa kienyeji anayedaiwa kufanya kitendo hicho kwa mgonjwa wake, baada ya mgonjwa huyo kufika kwake kwa lengo la kupata tiba ya maradhi yanayomsumbua, ndipo mganga aliingiwa na tamaa ya kimapenzi na kumpa dawa za kumpumbaza kisha kumbaka kwa kuweka baadhi ya dawa za kienyeji kwenye sehemu za siri za mwanamke huyo kama sehemu ya matibabu.

Mwenyekiti wa CHAWATIATA Kata ya Kishiri jijini Mwanza, Msabaha Salum, amekemea vikali kitendo alichofanya mganga huyo na kuomba Serikali kumchukulia hatua kali za kisheria.