Alhamisi , 19th Apr , 2018

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Job Ndugai amesema Bunge haliwezi kuidhinisha fedha kwa ajili ya matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwa kuwa halijapata vibali vitatu ambavyo vingemuwezesha kupata fedha za matibabu kutoka Bungeni.

Ndugai ametoa msimamo huo leo Aprili 19, 2018 Bungeni jijini Dodoma kwenye kikao cha 13 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya Mbunge Godbless Lema kuomba mwongozo wa kutaka kujua sababu zilizopelekea Bunge kutogharamia matibabu ya Mbunge huyo wa upinzani ambaye alipigwa risasi na watu wasiofahamika mwezi Septemba mwaka 2017.

"Utaratibu wetu katka nchi hii ni kwamba Mbunge akienda kutibiwa nje, lazima pawepo na barua kutoka kwa Rais, kibali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na Hospitali ya Taifa, Muhimbili kwamba mgonjwa fulani anahitajika rufaa tena wao ndio watasema apelekwe wapi ili Bunge liweze kuandika 'check' (hundi) aweze kupata fedha za matibabu. Bila ya hivyo Bunge haliwezi kufanya jambo lolote", amesema Spika Ndugai.

Mtazame hapa chini Spika wa Bunge, Job Ndugai akifafanua vizuri..