Mbatia achukuliwa fomu ya Ubunge, atoa neno

Jumatatu , 27th Jul , 2020

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha  NCCR-Mageuzi Jimbo la Vunjo, kwa kauli moja wamechanga fedha kiasi cha Sh 370,000 na kumchukulia fomu Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake James Mbatia kwa ajili ya kugombea ubunge kwa kipindi kingine.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Mbatia ameahidi kuwa atafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha maendeleo ya Jimbo hilo yanazidi kukua kwa kasi, na kuahidi kuwatumikia wananchi wa Jimbo hilo kwa nguvu zake zote.

''Kutoka sakafu ya moyo wangu ,nabeba dhamana  ya kugombea Ubunge wa Jimbo hili la Vunjo ,naahidi tutafanya kazi kwa pamoja usiku na mchana ili kutimiza yale yote ambayo mnayatamani yafanyike" amesema Mbatia.

Aidha ameongeza kuwa, "Vunjo ni yetu na niahidi kuwa Vunjo yetu itaendelea kung'ara na yale machache ambayo hatukuyakamilisha kutokana na changamoto za hapa na pale tutaenda kukamilisha".