Alhamisi , 14th Mar , 2019

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amewashukuru viongozi wa chama chake wakiwemo wabunge na wananchi ambao walijitokeza kumpigania ili kuhakikisha kiongozi huyo anatoka nje kwa dhamana.

Mbowe ametoa shukrani hizo baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya siku 100 baada ya kudaiwa kukiuka na masharti ya dhamana yeye pamoja na Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko katika kesi inayowakabili maarufu kama 'kesi ya Akwilina'.

Mbowe amesema kuwa, “natambua na kuheshimu mno ushiriki wenu kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na sala, ushauri, huduma ya chakula, michango ya fedha, na zaidi walioweza kutenga muda wao na kuja kututembelea na kutufariji gerezani".

Nitoe shukrani vilevile kwa wale wote waliotoa 'support' kwa familia  zetu na hata kututunzia na kujenga kwa njia mbalimbali majimbo yetu ya uchaguzi ikiwemo kazi  ya CHADEMA ni Msingi.” ameongeza Mbowe

Kwa wale walioshindwa vyote hivyo, watambue kwa dhati nawapenda na kuwaombea yote yaliyo mema na kama wapo waliokwazika kwa njia moja au nyingine pia nichukue fursa hii kuwaomba msamaha", Mbowe amemalizia katika taarifa hiyo.