Mbowe aweka wazi jambo jema katika bajeti

Jumanne , 13th Mar , 2018

Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amefunguka na kusema kuwa katika bajeti ya mwaka 2018/2019 serikali haijaongeza sana matumizi ukifananisha na bajeti ya 2017/2018. 

Mbowe amesema hayo leo Machi 13, 2018 akiwa mjini Dodoma baada ya Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango kuwasilisha mapendekezo ya serikali ya mpango wa maendeleo wa taifa na kiwango na ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2018/19.

"Jambo moja ambalo nafikiri ni jema kwenye bajeti hii serikali haikuongeza sana matumizi utaweza kuona kwamba imeongeza matumizi kutoka kwenye bajeti ya mwaka jana kutoka bilioni 740 tu tofauti na mwaka jana ambapo waliongeza bajeti kwa zaidi ya trilioni tano, hata katika kinachoitwa mipango ya miradi ya kielelezo bado kilimo hakipo katika miradi ya kielelezo na kilimo kinawahudumia wananchi wengi zaidi" alisema Mbowe 

Bunge la bajeti 2018/19 linatarajiwa kuanza vikao vyake Aprili 3, mwaka huu mjini Dodoma