Jumanne , 15th Oct , 2019

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema chama hicho kamwe hakitasusia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwataka Watanzania kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi huo.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Oktoba 15, 2019, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Jjijini Dar es salaam, ambapo amesema endapo Watanzania watasusia uchaguzi huo itakuwa ni athari kwenye maisha yao.

"Kuna watu wanasema CHADEMA na vyama vya Upinzani tususie uchaguzi na sisi tunaona sio sawa, kwa sababu wenzetu wanatamani tususie na niwaombe Watanzania wajitokeze kujiandikisha, mkisusia uchaqguzi maanake mmesusia maisha yenu". amesema Rais Magufuli

Aidha Mbowe amesema kuwa "uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa tusiuchukulie kiwepesi kwa sababu ni ikulu kwa wananchi, athari kubwa itakayotkana na huu uchaguzi, itakuwa na athari kubwa sana hapo baadaye, tutashiriki chaguzi za Serikali za Mitaa tutashinda na tutashinda sana".

Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo, juzi Oktoba 13, 2019, alitangaza kuongeza muda wa siku 3 kujiandikisha kwa wananchi, kwenye daftari la mpiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi huo.