Mbowe kugombea Uenyekiti, Lissu Makamu

Jumamosi , 30th Nov , 2019

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema atagombea Makamu Mwenyekiti wa chama hicho katika Uchaguzi unaoendelea kufanyika hivi sasa ndani ya chama hicho.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akirejesha fomu za kuwania Uenyekiti wa chama hicho kwa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini..

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe wakati akirejesha fomu yake ya kuwania Uenyekiti wa chama hicho. kwa Katibu wa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini.

Mbowe amesema kuwa "Sisi viongozi tunafahamiana historia zetu na umadhubuti wetu, baada ya mashauriano tumemuelekeza Tundu Lissu ajaze fomu ya kuomba nafasi ya Makamu Mwenyekiti, na amefanya hivyo japo hatuzuii mwingine yoyote kujaza nafasi hiyo"

"Kwa sababu Prof. Abdallah Safari (Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara) anaondoka, wamejitokeza Watanzania kadhaa kujaribu kugombea nafasi hiyo, kwa kuwa tunahitaji viongozi" amesema Mbowe

Kwa sasa chama hicho kimeingia kwenye Uchaguzi wake wa ndani ngazi ya Kikanda ambapo Desemba 18, ndiyo uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti utafanyika.