Mbowe na Nyalandu walivyoingia CCM Kirumba

Jumatatu , 9th Dec , 2019

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda yaKati, Lazaro Nyalandu wamewasili katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza,  kuhudhuria maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda yaKati, Lazaro Nyalandu wamewasili katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Taarifa ya kushiriki kwenye maadhimisho kwa Mwenyekiti wa CHADEMA ilitolewa juzi na Kamati Kuu ya chama hicho kwa kumuagiza Mwenyekiti wake kwenda kukiwakilisha chama hicho kwenye Sherehe hizo za Uhuru.

Katika Maadhimisho hayo Mbowe alifika asubuhi sana majira ya saa 2 kamili na na Waziri Jenister Muhagama na kelekezwa kukaa kwenye Jukwaa la watu watu mashuhuri.

Hii ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kushirii kwenye maadhimisho ya Uhuru tangu mwaka 2015.